Teuvo Kopra:

 

 

 

Ujumbe wa Ufunuo

 

 

Kwanza

 

Neno la Mungu lina utajiri mwingi.

Neno moja linaweza kuangaliwa kwa njia nyingi tofauti na tunapata mawazo ma­pya kwa neno hilo. Hii inatueleza ukuu wa Mungu na utajiri unaomo ndani ya Biblia. Akili za Mungu hatuzitambui ila kwa se­hemu ndogo. Ni hivyo hata katika Kitabu cha Ufunuo.

 

Kimefafanuliwa kwa njia tofauti. Pia inategemea hali yenyewe. Pia kuna tafsiri mbali mbali ambazo mtu mwenyewe ametafsiri kadri ya kuelewa kwake. Hizo hazijapewa msisimuko na Roho Mtaka­tifu lakini tunaweza kuzigundua na kuzie­lewa.

 

Tusingekuwa na Kita­bu cha Ufunuo ha­tu­ngeelewa yanayoendelea sasa. Hatungejua ubaya ulioko du­niani. Hatungeelewa ni kwa nini Mungu ana­kubali yale yanayotendeka duniani. Bila ya Kitabu cha Ufunuo hatungejua mwisho wa dhambi na shetani ingekuwa kwa utinyo sana kue­lewe. Lakini katika Ufunuo tunaambiwa kwamba kila kitu kibaya kina mwisho wake. Bila ya Kitabu cha Ufunuo hatungeelewa ku­husu vita, uhalifu na mateso makali ya nayowapata wanadamu.

 

Tukisoma Biblia tangu mwanzo mpaka mwisho tutaona kwamba Ufunuo ni kilele cha mambo yote ya Biblia. Tunaona katika Ufunuo kwamba sha­baha ya Mungu ni nini. Kitabu hiki kinawafariji wanaoudhiwa na kuteswa na wanaoona mateso ya aina mbali mbali kwa kumfuata Yesu. Pia katikati ya masumbufu ya kila siku, kitabu hiki kinatupa matumaini ya mambo yajayo kwamba siku moja huzuni yote itakwi­sha.

 

Tukiangalia huku na huku na kuona uovu ulivyozidi, mateso na kumdhihaki Mungu, tunajua kwamba mambo yatabadilika upesi. Wanaodhihaki watapata hu­kumu yao na ubaya pia sehemu yake. Wafuasi wa Yesu watapata thawabu na ma­zuri yajayo.

 

Wengine wanataka kupinga Kitabu hiki cha Ufunuo. Wao wanasema hayo ni mambo tu siyo kweli, hayatafanyika. Ni mifano tu.

Lakini tukisoma Biblia nzima tunaona kwamba, tabia ya Mungu iko kama mi­fano iliyotofautishwa na yale yali­yote­ndeka na sisi hatuwezi kuyachanganya. Pia hata yale ya kweli yana maana yake na hapo tunaona utajiri wa Biblia. Mambo mengine madogo katika Ufunuo ya­meshatimia, hata kwa kujirudia. Huo ni utangulizi. Matukio kamili na ya mwisho yatakuja baadaye, wakati ukifika. Sura zile za kwanza za Ufunuo zimekwi­sha ti­mia.

 

Sasa hivi tunaishi wakati wa unabii wa Mungu katika sura ile ya tatu.Wakati ule Yohana alipopata Ufunuo ka­tika kisiwa cha Patmo huo wote ulikuwa unabii. Baadhi ya mambo mengine yamekwisha timia. Yohana alitabiri nasi tutaangalia jinsi ufunuo huo ulivyolenga sawa.

 

 

 

Ufunuo 1.

 

Ufunuo aliyopewa Yohana

Salamu kwa makanisa saba

Njozi ya Mwana wa Mtu

 

Sura ya kwanza ni utambulisho wa Ufunuo mzima ufafanuzi na maelezo. Sura hii ni sura ya utangulizi, au dibaji. Tukisoma na kuamini yale yaliyoandikwa ka­tika sura hii hivyo yalivyoandikwa tu­nae­ndelea kuchunguza mambo mengine katika Ufunuo.

 

Hapo ndipo tutakapopata ujumbe ule ambao Roho Mtakatifu anataka kutupa. La­kini tukianza kuitafsiri kwa njia tofauti tangu mwanzo tukifikia mwisho tutaku­wa mbali na ukweli na kupotea kabisa.

 

1. Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awa­onye­she watu­mwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi; naye akatuma kwa mkono wa malaika aka­mwonyesha mtumwa wake Yohana; 2. aliye­lishuhu­dia Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu Kristo, yaani, mambo yote aliyo­yaona. (UFU 1:1,2)

 

Mungu alimpa Yesu Kitabu cha Ufunuo, ma­laika alikabidhi kwa Yohana naye akatua­ndikia sisi.

Kwa nini?

"awaonyeshe watu­mwa wake mambo amba­yo kwamba hayana budi kuwako upesi" (mst 1)

 

Yeye anawaonyesha watumishi wake - siyo ulimwengu. Ndiyo maana wasioamini hawawezi kukie­lewa Kitabu cha Ufunuo.

Tulisoma: "kwamba hayana budi kuwako upesi" (mst 1)

 

Wakati wa ku­patikana kwa kitabu hiki mambo yalikuwa yameshaanza. Wakati wa makanisa uli­kuwa tayari. Lakini baada ya wakati wa makanisa matukio mengine yatafanyika upesi na kwa muda mfupi sana.

 

3. Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuya­shika yaliyo­andikwa humo; kwa maana wa­kati u karibu. (UFU 1:3)

 

Tunaposoma Kitabu hiki uheri wetu una­o­ngezeka ingawa hatuelewi kila kitu.Uheri unaongezeka zaidi kadiri ya kuele­wa kwetu ujumbe huo. Pia kama ujumbe huo utapata nafasi ndani ya maisha yetu uheri unazidi zaidi. Ndiyo maana tungependa kusikia ujumbe huo mioyoni mwetu na siyo tu kwa ma­sikio.

 

4. Yohana, kwa yale makanisa saba yaliyoko Asia; Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwake yeye aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja; na zi­tokazo kwa roho saba walioko mbele ya kiti chake cha enzi; 5. tena zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi aliye mwaminifu mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Yeye atu­pendaye na kutu­osha dhambi zetu katika damu yake, 6. na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu, naye ni Baba yake; utu­kufu na ukuu una Yeye hata milele na milele. Amina. (UFU 1:4-6)

 

Mistari hii ni kwa makanisa saba. Yohana alichapisha barua saba za Ufunuo kwa kila kanisa barua moja. Lakini kwa sababu Ufunuo uko katika Biblia mambo hayo yanatuhusu sisi pia, na siyo ma­kanisa saba ya Asia tu.

 

Tulisoma kwamba Yesu ku­tuosha dhambi zetu katika damu yake. (mst 5) Ili tuelewe kitabu hiki lazima tue­lewa ku­husu upatanisho ambao umefanyika kwa sababu ya upendo kwa ajili ya wenye dhambi na pia wanaoishi katikati ya hu­kumu ya Ufunuo.

 

Yesu ni "mkuu wa wafalme wa dunia." Mwingine anasema kwamba wala haifa­nani hivyo. Lakini Yesu ndiye mwamuzi na anaye­weka mipaka kwa waovu hata wana­shindwa kui­vuka. Ni lazima dunia ijiandae kwa hukumu, ndiyo maana hata wabaya wanaachi­wa uhuru wa kuyafanya mambo yao. Lakini ni kwa muda uliyowekwa tu.

 

4. Bwana amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya. (MIT 16:4)

 

Matukio katika Kitabu cha Ufunuo haya­wezi kutokea iwapo ubaya haupo. Wapa­gani wanahitajika ili malengo na hu­kumu ya Mungu viweze kutimia. Ubaya utaka­poenea zaidi au unatosha, Mungu atau­maliza. Tulisoma: ... na kutufanya kuwa ufalme, na ma­kuhani kwa Mungu. (mst 6) Bado hatuna ufalme unaoonekana, lakini tu­naambiwa katika Ufunuo utakavyokuja na utachukua muda gani.

 

Pia Ufunuo inatueleza ni nani watakaota­wala huko na utachukua muda gani na utageukaje kuwa ufalme wa milele, yaani Mbingu mpya.

 

7. Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho lita­mwona, na hao walio­mchoma; na kabila zote za dunia wataombo­leza kwa ajili yake. Naam. Amina. (UFU 1:7)

 

Hapa tunaelezwa kurudi kwa Yesu. Sisi pia tunaongelea mara kwa mara jambo hili. Hapa hatuelezwi kurudi kwa Yesu tuna­koku­subiri sasa, ila ni yale tuliyoandi­kiwa katika Ufunuo sura ya kumi na tisa. Kuja kwa Yesu tunakokusubiri kutafa­nyika kabla ya kurudi kwake, kama tuli­vyosoma ni wakati ambapo wote wata­mwona na wakati huo pia ataanzisha utawala wake wa miaka elfu moja ya amani hapa duniani.

 

Yesu atarudi, kama tunavyokusubiri ku­rudi kwake kutatokea ghafla na hivyo hawataona kwa macho. Juu ya kurudi kwa Yesu tunakokusubiri sasa, tu­some sehemu mbili katika Biblia.

 

16. Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kuto­ka mbi­nguni pamoja na mwali­ko, na sauti ya malai­ka mkuu, na parapanda ya Mungu; nao wali­okufa katika Kristo wata­fufuliwa kwanza. 17. Kisha sisi tu­lio hai, tulio­salia, tu­tanya­kuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana he­wani; na hivyo tuta­kuwa pamo­ja na Bwana mi­lele. (UFU 1:16,17)

 

Yaani kwanza Yesu atarudi na waliooko­ka waliokufa watafufuliwa. Yaani miili yao iliyozikwa itafufuka. Halafu wale waliohai yaani wakristo wa­tanyakuliwa kwenda kumlaki Bwana mawi­nguni. Baada ya hapo tutakaa naye milele. Kwanza kwenye harusi Mbinguni baa­daye hapa duniani katika utawala wa Mungu wa mia­ka elfu moja.

Baadaye milele Mbinguni.

 

51. Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, la­kini sote tuta­badilika, 52. kwa dakika moja kufumba na kufubua, wakati wa parapa­nda ya mwisho; maana para­panda italia, na wafu watafufu­liwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. (1KOR 15:51,52)

 

Wale wakristo waliokoka hapa wakati wa kurudi Yesu hawataonja mauti bali wa­ta­badilika. Mabadiliko haya ni makubwa na yako sawa au yanakaribiana na kifo na ufufuo. Haya yatatokea ghafla kufumba na kufu­mbua. Hapa tunaambiwa kuhusu unyakuo, ambao utatokea kwa gha­fla na kwa siri sana. Wakati ule yeye hatafunuliwa kwa uli­mwengu. Lakini Ufunuo sura ya kwanza mstari wa saba inatuambia kwamba kurudi kwake dunia nzima watamwona. Yeye hatakuja kunyakua bali kuanzisha uta­wala wa amani hapa duni­ani. Ataandamana na bibi arusi ambaye ata­kuwa amekwisha nyakuliwa.

 

8. Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliekuwako na atakayekuja, Mwenyezi. (UFU 1:8)

 

Msemo "Alfa na Omega" kwa Kiebrania una maana ya herufi ya kwanza na ya mwisho katika alfabeti. Sisi tungeweza kusema "A na Z". Mwanzo na mwisho na herufi zingine hapa katikati. Mungu ni wa zamani, sasa na wakati ujao.

 

9. Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na subira ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu. (UFU 1:9)

 

Wakati Kitabu cha Ufunuo kilipoandikwa kaisari Domitiani alikuwa akitawala. Wakati huo dunia nzima ilikuwa chini ya utawala wa Rumi. Kaisari Domitiani alitawala mwaka wa the­manini na moja mpaka tisini na sita baada ya Kristo. Ali­kuwa anapinga imani ya Kikristo na pia alikuwa mtesaji. Ndiyo maana alitoa amri Yohana apele­kwe kisiwa kilichoitwa Patmo. Sikuhizi kinaitwa Patino. Baada ya kaisari Domitiani kaisari Nerva alitawala dunia nzima.

Alitawala Rumi mwaka wa tisini na sita mpaka tisini na nane baada ya Kristo. Yeye alikubali Injili na hata akamtoa Yo­hana kule kisiwani.

 

Tunaona kwamba Mungu alimweka mamla­kani kaisari aliyempinga Yohana na ku­mweka kisiwani ili aweze kupokea ujumbe wa Ufunuo huko. Kwa hivyo kaisari Domitiani alihusika ili Yohana apate Ujumbe. Baada ya Ujumbe kupatikana kaisari alito­lewa mamla­kani na Mungu alihitaji kaisari mwingine aliyemleta Yohana pamoja na ule ujumbe wa Ufunuo kwa watu. Hapa tunagundua kwamba ni Mungu anayeamua kuhusu utawala wo wote ule wa wafalme hata serikalini. Wao wanaabudu mipango miku­bwa ya Mungu. Yeye anamwinua fulani kutawala na ku­mwondoa mwingine.

 

Patmo yaani Patino ni kisiwa kidogo kama kilomita arobaini za mraba. Huko Yo­hana alikuwa peke yake na ali­weza kupewa ujumbe huo wa Ufunuo.

 

10. Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu, (UFU 1:10)

 

Ninafikiri kwamba hapa "siku ya Bwana" ni Jumapili. Tangu wakati wa mitume Jumapili ilishe­re­hekewa kama siku ya kufufuka kwa Yesu. (MDO 20:7) Yaani siku ya Bwana Yesu Kristo alipofu­fuka kutoka wafu baada ya kusu­lubiwa. Katika se­hemu zingine siku ya Bwana maana yake ni siku ile ya ghadhabu. (2THE 2:2, YOE 2:1-11, ISA 13:9-13, AMO 5:18-20, SEF 1:14-18)

Yohana alipo­kuwa kisiwani siku ya Ju­mapili alisikia sauti kubwa ambayo bila shaka alii­fahamu.

 

11. ikisema, Haya uyaonayo uyaandike katika chuo, uka­yapeleke kwa hayo ma­kanisa saba Efeso, na Smirna, na Pergamo na Thiatira, na Sardi, na Fila­delfia, na Laodi­kia. 12. Nikageuka niione ile sauti iliyosema nami. Na nilipo­geuka, nili­ona vinara vya taa saba vya dhahabu; 13. na katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa Mwana­damu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa mshipi wa dhahabu matitini. 14. Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe, kama theluji; na macho yake kama mwali wa moto; 15. na mi­guu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanu­ru; na sauti yake kama sauti ya maji mengi. 16. Naye ali­kuwa na nyota saba kati­ka mkono wake wa kuume; na upanga mkali, wenye ma­kali kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua li­king´aa kwa nguvu zake. (UFU 1:11-16)

 

Kumbe Yohana alisikia sauti kama ya bara­gumu. Aliona katika maono vinara saba vya dhababu. Na katikati ya vile vinara aliona mtu mfano wa Mwanadamu, yaani Yesu na nyota saba hayo yote yalikuwa katika mkono wa kulia wa Yesu. Hata ingawa Yohana alikuwa amemwona Yesu hapo awali, ameegemea kifuani mwake wakati wa chakula cha mwisho na pia ali­mwona baada ya kufufuka kwake, maono hayo yalikuwa na nguvu sana alishindwa kustahimili. Hapo awali Yesu alikuja hapa duniani na Yohana alikuwa mmoja wa wanafunzi wake, Yesu hapa duniani aliku­wa kama mtumwa, akawa kama mwanadamu. Lakini sasa alichukuwa mwili wake wa utu­kufu ndiyo maana Yohana alishindwa ku­mwangalia. Na sasa Yohana ana­tueleza hali aliyo­kuwa nayo baada ya kuona yale maono.

 

17. Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho, 18. na aliye hai; nami nali­kuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu. (UFU 1:17,18)

 

Yesu alisema: "Usiogope!" Hatuna haja ya kuogopa mambo haya kwenye Ufunuo hasa waliookoka. Kama mahubiri yetu yatawafanya watu wao­gope inamaana kwamba hatujafau­lu katika kutafsiri na kuchunguza Ufunuo. Tumekosea.

 

Sasa tusome sehemu muhimu sana mstari wa kumi na tisa.

19. Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo yali­yopo, na yale yatakayo­kuwa baada ya hayo. (UFU 1:19)

 

Mstari huu tunaweza kuutumia kama ufunguo katika kutafsiri Ufunuo. Kama tutatumia mstari huu kutafsiri Kita­bu kizima tutapata tafsiri iliyosahihi.

 

Mstari huo una sehemu tatu:

Kwanza: Uandike uliyoyaona, yaani Yo­hana ali­mwona Yesu, vinara vya taa saba na zile nyota saba.

Pili: Uandike .. nayo yaliyo­po. Yaani ni wakati gani unaendelea sasa, wakati Yohana alipokuwa Patmo. Uli­kuwa wakati wa makanisa. Wakati wa makanisa ulianza tangu siku ile ya Pente­koste na kuendelea wakati wa ma­tukio huko katika kisiwa cha Patmo kama miaka sitini. Siku hizi wakati wa makanisa bado una­ende­lea. Ufunuo sura za pili na tatu zinatue­leza juu ya wakati wa makanisa.

Na mambo ya tatu yalikuwa: Uandi­ke.. yale yatakayokuwa baada ya hayo. Yaani ni nini kitakachotokea baada ya hapo kitugani kitatokea baada ya wakati huo wa makanisa, mambo hayo Yohana aliandika ka­tika sura ya nne mpaka sura ya ishirini na mbili.

 

20. Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dha­habu. Zile nyota saba ni malaika wa yale ma­kanisa saba; na vile vinara saba ni makanisa saba. (UFU 1:20)

 

Zile nyota saba ni wahubiri, wazee wa makanisa na viongozi wengine makanisani. Vile vinara saba vina maana ya makanisa ya palepale. Kinara kimoja ni kanisa moja. Biblia inatueleza katika Agano la Kale zaidi kuhusu kinara. Hapo kuna taa saba zi­nazowekwa ma­hali pake. Mtu anapookoka taa yake inawashwa. Mafuta ni uhai wa Mungu, taa ni mioyo yetu. Yesu alizumgumzia kiango na taa katika In­jili ya Ma­thayo.

 

15. Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. (MT 5:15)

 

Tuliposoma, kwamba kiango ni mfano wa kanisa la pale pale, tunagundua kwamba Yesu alitaka kusema kwamba mtu ana­poo­koka mahali pake ni kwenye kiango yaani kanisani.

 

Endelea sura ya 2.

 

Ujumbe kwa Efeso

Ujumbe kwa Smirna

Ujumbe kwa Pergamo

Ujumbe kwa Thiatira

 

-------------------------------------------------------------------------

 

 

 

(Hubiri 801)